Halmashauri ya Manispaa Sumabwanga kupitia
Idara ya Maendeleo ya Jamii iliandaa Kongamano la Uwezeshaji Kiuchumi kwa
Wanawake Wajasiriamali ndani ya Manispaa ya Sumbawanga. Kulingana na fomu ya
mahudhurio Kongamano hilo lililofanyika tarehe 15/11/2019 lilihudhuriwa na
Wanawake Wajasiriamali 657 sawa na 164 ya lengo la kuwafikia Wananwake 400.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa kutoka
kwa Wataalam wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), Idara ya Kilimo, Idara ya Mifugo na Uvuvi, Taasisi ya PASS (Private
Agricultural Sector Support) Shirika la Viwanda Vidogo la SIDO – Rukwa, TBS
ofisi ya Kanda Mbeya na Benki za NMB na CRDB.
Pia
katika Kongamano hilo walihudhuria Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya
Sumbawanga Mjini wakiongozwa na Katibu Mhe. Said King’eng’ena, pamoja naye
walikuwepo Viongozi wa Jumuiya za Chama ambao walipata fursa za kutoa Salaam za
Chama na kueleza shunguli na miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Nchini na
Serikali ya Awamu ya Tano.
1.0.
MADHUMUNI
YA KONGAMANO
Kongamano la Uwezeshaji Kiuchumi la
Wananwake Wajasiriamali lilifanyika kwa ajili ya kuamsha Ari kwa Wanawake
Wajasiriamali wa Manispaa ya Sumbawanga na kuwajengea Uwezo wa Kutambua fursa
mbalimbali zilizopo ndani ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na dhamana na nafasi
yao katika Ujenzi wa Taifa.
2.0.
MALENGO MAHSUSI.
Malengo mahususi ya Kongamano la Uwezeshaji
Kiuchumi la Wanawake Wajasiriamali ilikuwa ni pamoja na:- lililenga hasa katika
kufikia malengo mahsusi yafuatayo:-
·
Kuwa na Kongamano la kuwakutanisha
Wananwake Wajasiriamali wa Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya kubadilishana
uzoefu.
·
Kuwaonesha wanawake Wajasiriamali fursa
zinazopatikana katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
·
Kutambua
changamoto wanazokutana nazo na kwa pamoja kutafuta ufumbuzi wa kuzitatua
changamoto hizo.
·
Kuwafanya wanawake kutambua fursa ya mikopo
inayotolewa na Halmashauri kupitia 10% ya mapato ya ndani ili waweze kupata
mitaji na kuanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi.
·
Kuwafanya wanawake kufahamiana na
kubadilishana uzoefu ili kujenga hali ya uthubutu, kujituma na kuwekeza katika
Ujasiriamali.
·
Kuwaunganisha wanawake na fursa mbalimbali
za Kiuchumi zinazopatikana ndani ya Manispaa ya Sumbawanga zikiwemo kilimo,
ufugaji, biashara na mikopo kutoka kwenye Taasisi za Kifedha.





